Kifo cha hayati Navalny chaiweka Russia katikati ya siasa za Marekani

  • VOA News

Alexey Navalny

Kifo cha kiongozi wa upinzani Russia, Alexei Navalny kimeiweka Russia katikati ya siasa za Marekani na kuongeza shinikizo kutoka kwa Warepublican katika bunge kuiunga mkono Ukraine.

Wakati huo huo rais Joe Biden na mpinzani wake mkuu, rais wa zamani Donald Trump, wakiwa na maoni tofauti kuelekea uchaguzi wa rais mwezi Novemba.

Wagombea hao wawili wameingia katika majadiliajo kuhusu uchaguzi wa rais wa Marekani.

Kifo cha kiongozi wa upinzani Alexey Navalny katika gereza moja huko Russia kimeongeza matamshi ya kisaisa ya Marekani kuhusu Rais wa Russia, Vladimir Putin na uvamizi wake nchini Ukraine, ikionyesha mgawanyiko wa dhahiri kati ya Rais Joe Bide na mpinzani wake mkuu wa urais, Donald Trump.

Biden amekuwa haraka kutoa lawama na kutishia vikwazo vikali kwa kifo cha Navalny katika gereza la Arctic, ambapo maafisa wa Russia wanaeleza ugonjwa uliosababisha kifo cha ghafla.

Rais wa Marekani Joe Biden

President Joe asema: “Ukweli wa mambo, Putin anahusika. Iwe alitoa amri, lakini anahusika kwa jinsi alivyomuweka mtu huyo. Ni ishara ya huyu ni mtu wa aina gani. Hili haliwezi kustahmiliwa. Nasema kuna gharama ya kulipa.”

Kremlin imesema shutuma hizo hazina msingi na za kijeuri na mamlaka imemnyima mama yake fursa ya kuuona mwili wake.

Trump na chama chake cha Republican wamechukua mwelekeo tofauti, huku Trump akisema hataiunga mkono NATO kama anavyofanya Biden. Katika tukio la karibuni kwenye Fox News, alijitaja kuwa ni muathirika wa mashtaka ya kisiasa kama Navalny.

Donald Trump aeleza: “Ni jambo baya sana, lakini linatokea katika nchi yetu pia. Tunaigeuza nchi kuwa ya kikomunisti kwa njia nyingi. Kama ukiangalia, , mimi nimgombea ninayeongoza. Sijawahi kusikia kushtakiwa hapo kabla, nimeshtakiwa mara nne, nina kesi nane au tisa, yote kwasababu unajua yote haya yanahusu siasa .”

Trump hakufafanua jinsi atakavyomaliza vita vya Russia nchini Ukraine badala yake amesema kwamba kama angekuwa rais, Putin kamwe asingeivamia Ukraine.

Rais wa Marekani Joe Biden alipokutana na Rais wa Russia Vladimir Putin mwaka 2021 huko Geneva, Uswiss.

Warepublican wamehoji kwanini wafadhili mzozo. Majeshi ya Russia hivi karibuni yaliukamata mji muhimu, ambao White House inaeleze ni ushahidi kwamba majeshi ya Ukraine yanahitaji msaada wa haraka.

Baadhi ya Warepublican wana imani kuwa watapitisha msaada uliokwama wa dola bilioni 95. Msaada mwingi ni kwa ajili ya Ukraine.

Wakati huo huo vita vimechukua umuhimu mkubwa sana. Peter Pomerantsev wa chuo kikuu cha Johns Hopkins anasema , “ hili limekuwa ni kuhusu Mareknai. Je Marekani inataka kuendelea kuwa na jukumu la juu katika kutimiza ahadi zake, ambazo zinaheshimu ushirika ilio nao na kwamba zina uwezo wa kuonyesha nguvuyake? au nguvu ya Marekani imekwisha? Hilo ndiyo swali la hivi sasa. Si tena kuhusu Russia au Ukraine.

Moscow na Washington wako umbali wa karibu kilometa 8,000.

Lakini wakati Marekani inaelekea Novemba, hatima yao imefungamana zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali.

Ripoti ya mwandishi wa VOA Anita Powell