Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 01:24

Familia ya Navalny yadai kuzuiliwa kuuona mwili wake


Mke wa Alexei Navalny, Yulia Navalnaya akizungumza mbele ya mawaziri wa mambo ya kigeni wa EU, mjini Brussels.
Mke wa Alexei Navalny, Yulia Navalnaya akizungumza mbele ya mawaziri wa mambo ya kigeni wa EU, mjini Brussels.

Mke wa kiongozi wa upinzani wa Russia Alexei Navalny amemtuhumu Rais Vladimir Putin kwa mauwaji ya mumewe na ameahidi kutaja majina ya wale anaodai walihusika na kifo chake.

Tuhuma hizo kwenye video zimetolewa baada ya mamake Alexei, Lyudmila kusema kuwa amezuiliwa kuuona mwili wake kwa siku ya tatu mfululizo, wakati ikulu ya Kremlin ikisema uchunguzi kutokana na kifo chake unaendelea.

Kifo cha Navalny akiwa kwenye gereza moja ya Russia wiki iliopita kimeshtua viongozi wa upinzani wa Russia waliokimbilia mataifa ya kigeni, pamoja na mataifa ya magharibi, wakati kidole cha lawama kikielekezwa kwa Kremlin.

Yulia Navalny Jumatatu amekutana na Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, Charles Michel mjini Brussels, baada ya kutoa tuhuma zake dhidi ya Putin na baada ya waziri wa mambo ya nje wa Ujeruimani Annalena Baebock, kusema kwamba atapendekeza vikwazo vipya dhidi ya Moscow kutokana na kifo cha Navalny

Forum

XS
SM
MD
LG