Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 03:15

Kifo cha Navalnay chaacha pengo kubwa kwa upinzani Russia


Waandamanaji wakiwa wameshikilia bango linalosomeka "Tutaendelea" mbele ya ubalozi wa Russia mjini Berlin, Februari 18, 2024 wakati wa maombolezo ya kifo cha Alexei Navalny.
Waandamanaji wakiwa wameshikilia bango linalosomeka "Tutaendelea" mbele ya ubalozi wa Russia mjini Berlin, Februari 18, 2024 wakati wa maombolezo ya kifo cha Alexei Navalny.

Kifo cha ghafla cha mpinzani mkubwa wa rais wa Russia Vladimir Putin kimeacha pengo kubwa kwa upinzani wa kisiasa wa nchini Russia.

Alexei Navalnay mwenye umri wa miaka 47, alikuwa mkosoaji maarufu wa Kremlin, ndani na nje ya nchi. Kabla ya kifo chake wakati akitumikia adhabu ya kifungo katika gereza lililoko kaskazini mwa Arctic siku ya Ijumaa. Maisha ya mtetezi huyo mkuu wa vita dhidi ya ufisadi, mratibu wa maandamano na mwanasiasa mwenye hisia za ucheshi ilimulikwa kwenye filamu iliyoshinda tunzo.

Katika kurasa zake za YouTube alikuwa na mamilioni ya watu waliojisajili.

Navalny pia alikuwa kiongozi wa kwanza wa Russia kupokea kifungo cha muda mrefu katika miaka ya hivi karibuni. Kutakuwa na wengine, kutokana na unyanyasaji dhidi ya wapinzani wanaokosowa uvamizi wa Ukraine.

Katika kipindi cha miaka mitatu tangu Navalny apoteze uhuru wake, wapinzani kadhaa wamekuwa wakifungwa, wakati wengine walilazimika kukimbia kutoka Russia kutokana na shinikizo la kisiasa.

Washirika wake wa karibu – mwanamkakati mkuu Leonid Volkov, mkuu wa uchunguzi Maria Pevchikh, mkurugenzi wa tasisisi Ivan Zhdanov na msemaji Kira Yarmysh— pia wanakabiliwa na shinikizo na tishio la kuhukumiwa huko Russia.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP

Forum

XS
SM
MD
LG