Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, mtu yeyote anayeingia au kuondoka Algeria atahitajika kuonyesha kibali hicho.
Kibali hicho pia kitahitajika kabla ya kuingia kwenye viwanja vya michezo, kumbi za filamu na makumbusho miongoni mwa maeneo mengine muhimu.
Ni chini ya robo ya watu nchini Algeria ambao wamepokea walau chanjo moja kufikia sasa, na kwa hivyo inaonekana kwamba kuna kibarua kigumu cha kujaribu kutoa chanjo kwa watu zaidi.
Serikali imesema kwamba hatua hiyo mpya inalenga kukabiliana na wimbi jipya la maambukizi ya corona kutokana na virusi vya delta.Kufikia sasa ni kesi mbili pekee za aina mpya ya virusi vya omicron ambazo zimeripotiwa nchini Algeria. Serikali imesema kwamba itaongeza hatua zaidi katika siku zijazo ili kukabiliana na janga hilo