Kenya yatia saini mkataba wa kusambaza umeme na kampuni ya Adani ya India

Picha maktaba ya nyaya za umeme.

Kenya imetoa kadarasi ya usambazaji wa umeme kupitia ushirikiano na sekta ya kibinafsi na kampuni ya Adani ya India, pamoja na benki ya Maendeleo ya Afrika, kulingana na mshauri mkuu wa kiuchumi wa rais, David Ndii.

Kwa mijibu wa shirika la habari la Reuters, mkataba huo utagharimu dola bilioni 1.3, Ndii amesema Jumapili, kupitia ukurasa wake wa X. Kampuni ya Adani pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika kufikia sasa hawajasema lolote kuhusiana na mkataba huo.

Mpango tofauti kati ya serikali ya Kenya na kampuni ya Adani wa kukarabati uwanja wa kimataifa wa ndege wa Kenyatta umezua ghadhabu miongoni mwa wakenya, na kupelekea mgomo ulioitishwa na wafanyakazi wa uwanja huo.

Kampuni hiyo inasemekana kuendesha viwanja 7 nchini India, suala ambalo limekuwa likilalamikiwa na upinzani nchini humo, ingawa imekanusha shutuma hizo.