Hilo limefanyika licha ya shirika la Amnesty International kuelezea wasiwasi kuwa wanaweza kukabiliwa na mateso nyumbani ikiwa watafukuzwa nchini.
Ilikubali ombi la kuwafukuza kwa sababu ya uhusiano wenye nguvu kati ya nchi hizo mbili, taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Masuala ya Diaspora ilisema, na kuongeza kuwa ilipata uhakikisho kwamba watu hao wanne watatendewa kwa heshima kwa kuzingatia sheria za kitaifa na kimataifa.
Amnesty ilisema Jumamosi kwamba ikiwa watafukuzwa wanaweza kukabiliwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, ambao ilisisitiza wasiwasi unaoongezeka kuhusu usalama wa wakimbizi wote na wanaotafuta hifadhi nchini Kenya.
Kenya ilisema imejitolea kuwalinda wakimbizi wapatao 780,000 inaowahifadhi, wengi wao wakiwa wanatokea nchini Somalia.