Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 22, 2024 Local time: 22:25

Rigathi Gachagua amshutumu Rais Ruto wa Kenya ni mtu mbaya na mkatili


Rigathi Gachagua, Naibu Rais wa kenya aliyeondolewa madarakani hivi karibuni kufuatia kura ya wabunge ya kutokuwa na imani nae.
Rigathi Gachagua, Naibu Rais wa kenya aliyeondolewa madarakani hivi karibuni kufuatia kura ya wabunge ya kutokuwa na imani nae.

Gachagua aliondolewa madarakani  na Seneti kwa mashtaka matano kati ya 11 yaliyowasilishwa dhidi yake siku ya Alhamis.

Naibu Rais aliyeondolewa mamlakani nchini Kenya Rigathi Gachagua leo Jumapili alimshamblia mkuu wake William Ruto akisema ni “mbaya sana” na mkatili, akionya kuwa maisha yake yanaweza kuwa hatarini.

Gachagua aliondolewa madarakani na Seneti kwa mashtaka matano kati ya 11 yaliyowasilishwa dhidi yake siku ya Alhamisi, lakini amri ya mahakama ilizuia mchakato kumpata mrithi wa nafasi yake.

“Nimeshtushwa na jinsi mtu huyu mwenye roho mbaya niliyemsaidia kuwa rais, niliyemuamini na niliteseka wakati nilipomuunga mkono, anaweza kuwa na roho mbaya sana dhidi yangu, aliwaambia waandishi wa habari. Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 59 alisema ameondolewa ulinzi yeye na wafanyakazi wake wote wamepewa likizo ya lazima.

Kama chochote kitanitokea mimi au familia yangu, Rais William Ruto lazima awajibishwe, alisema, akidai majaribio ya zamani yaliyofanywa kwa maisha yake. Alikuwa akizungumza baada ya kutoka hospitali moja jijini Nairobi alikokuwa akitibiwa kutokana na maumivu makali ya kifua.

Forum

XS
SM
MD
LG