Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, taifa hilo la Afrika Mashariki pamoja na maafisa wa IMF walitangaza kukubaliana kuhusu tathmini ya 7 ya program ya dola bilioni 3.6 hapo Juni, lakini kukamilika kwa tathmini za mwisho kuelekea kutolewa kwa fedha hizo kulitatizwa na maandamano ya kitaifa. Zaidi ya watu 60 walikufa kwenye maandamano yaliopelekea Rais William Ruto kusitisha msuada wa fedha uliopendekeza kuongeza ushuru.
Uchumi wa Kenya hata hivyo umeendelea kubaki imara kulinganishwa na wastani wa kieneo, wakati mfumuko wa bei ukipungua, huku fedha za kigeni zikisaidia kuimarisha shilingi licha ya mazingira magumu ya kiuchumi yaliopo. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi naibu wa kwanza wa IMF, Gita Gopinath, kupitia taarifa ya Jumatano.
IMF pia ilisisitiza kuwepo kwa utawala mwema na uwazi kwenye serikali ya Kenya. Msaada wa IMF ni muhimu kwa Kenya ili iweze kukabiliana na upungufu wa fedha uliopo, uliopelekewa na viwango vya juu vya riba kwenye mikopo ya nje.