Kwa mujibu wa mtandao wa Citizen Digital, mratibu wa mamlaka ya kilimo na chakula ya Kenya (AFA) Alfred Busolo amesema parachichi ni tunda muhimu ambalo Wakenya wengi wanatumia wanapokula chakula.
AFA inasema kuwa upungufu ulioko unatokana na kuwa huu sio msimu wa Avocado zinazopendwa aina ya Faurte na Haas.
Kutokana na upungufu huo bei ya tunda hilo maarufu linalofahamika kama Avocado imepanda sana.
Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa katika jarida la Bussines Daily Nation la Kenya mapema wiki hii, kilo 90 za tunda hilo ilikuwa zinagharimu shilingi 2,560 za Kenya kufikia Disemba 2017.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo May 2017 kilo sawa na hizo ziligharimu shilingi 2,700.
Busolo anasema kuwa bei ya parachichi inatarajiwa kushuka mwezi ujao wakati wa msimu wa Fuerte huku aina ya Haas ikianza kuingia sikoni mwezi machi 2018.