Noordin Haji mkurugenzi wa mashataka ya umma: “Kanuni ya adhabu inaweza isitoshe lakini tutaangalia na kuona kulingana na aina gani ya ushahidi tunaoupata ili kuturuhusu kupeleka mashtaka yanayoendana na uhalifu ambao umetokea hapa, ambao ni wa kutisha. Kwa kuanzia pengine tutazingatia hata kumshitaki mtu huyo kwa uhalifu unaohusiana na ugaidi kama vile itikadi kali.”
Vyanzo vya habari vya polisi vimeiambia AFP jana jioni kuwa idadi ya vifo imefikia 73 wakati watu kadhaa wakiwa wameokolewa na kupelekwa hospitali.
Ugunduzi huo wa kusikitisha umeleta mshtuko kote nchini na kumfanya rais William Ruto kuaahidi kupambana na vuguvugu la dini zisizokubalika kukiwa na hofu kwamba idadi ya watu walioathiriwa inatarajiwa kuongezeka zaidi.
Inaaminika kwamba wafuasi wa kanisa la Good News International wanaweza kuwa bado wamejificha katika msitu wa Shakahola na wako katika hatari ya kifo ikiwa hawatapatikana haraka.