Picha zilizochapishwa kwenye mitandao ya X na vyombo vya habari vya Kenya, Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya na mamlaka ya barabara kuu zimeonyesha matukio ya baada ya mafuriko, miti iliyokatika na gari moja lililokwama kwenye magogo na matope.
“Kufikia sasa, tumefanikiwa kupata miili 42, ikiwemo miili ya watoto 17, kufuatia tukio la asubuhi ambapo bwawa lilipasua kingo zake eneo la Kijabe na shughuli za uokoaji na utafutaji zinaendelea,” kamanda wa polisi wa Naivasha Stephen Kirui amewambia waandishi wa habari kwenye eneo la uokoaji.
Mapema Jumatatu, Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limesema liliwapeleka watu kadhaa kwenye kituo cha afya huko Mai Mahiu kutokana na mafuriko.
Idadi ya vifo kutokana na mvua kubwa na mafuriko tangu mwezi uliopita imefikia zaidi ya 140.