Kauli mbiu ya WHO 2023: “Ni wakati wa kutokomeza malaria: wekeza, buni na tekeleza

FILE PHOTO: Matshidiso Moeti.

Aprili 25 kila mwaka, ulimwengu unaadhimisha Siku ya Malaria Duniani, mwaka huu yakiwa ni maadhimisho ya 16.

Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema ni wakati muafaka kuzingatia athari za madhara yanayotokana na ugonjwa wa malaria kwa maisha ya watu na maendeleo ya kiuchumi katika Kanda ya Afrika.

Mwaka 2021, kwa sababu ya hatua za pamoja zilizochukuliwa na nchi zilizoathiriwa na malaria na washirika wake, vifo vinavyotokana na malaria vilipungua ukilinganisha na 2020 licha ya kuwepo kwa athari za janga la COVID-19.

Juhudi hiyo inaungwa mkono na katika kauli mbiu ya WHO mwaka huu: “Ni wakati wa kutokomeza malaria: wekeza, buni na tekeleza.

Ujumbe wa Shirika la Afya Duniani (WHO) unasema kuwa Malaria imekuwa ni adui sugu wa afya ya umma.

Kulingana na Mkurugenzi wa WHO wa Kanda ya Afrika, Dkt Matshidiso Moeti. Mwaka 2021 malaria iliuwa watu 619,000, takriban asilimia 96 ya watu hao walikuwa wanaishi Afrika.

Kuna uwezekano wa mara sita mpaka 20 wa kuenea katika mazingira hatarishi ya mazalia ya mbu kuliko ilivyo kwa virusi vya Omicron vya Sar-cov-2.

WHO inasema kulikuwa na wakati ambapo ugonjwa wa malaria ulikuwa umeenea katika jamii sehemu kubwa ya ulimwengu.

Alieleza kuwa hivi sasa “tunaweza kuokoa maisha ya mamilioni ya watu kila mwaka kutokana na ugonjwa huu na vifo vinavyo sababishwa na malaria kufuatia hatua mpya tulizopiga katika kutokomeza ugonjwa huu.”

Chanzo cha habari hii ni Shirika la Afya Duniani, WHO.