Mbu wanasambaza ugonjwa wa Malaria ambao unaua zaidi ya watu laki sita kila mwaka. Idadi kubwa ya watoto barani Afrika chini ya jangwa la Sahara ndiyo waathirika wakuu. Taarifa iliyotolewa Jumatano na chuo kikuu cha Oxford inasema kuwa chanjo mpya ya malaria inayojulikana kama R21 imepata idhini ya bodi ya udhibiti iliyotolewa na maafisa wa Ghana kwa ajili ya matumizi kwa kundi maalum la watu ambao wako katika hatari ya kifo kutokana na malaria – ni watoto kati ya umri wa miezi mitano mpaka miezi 36.
Malaria ni ugonjwa ambao umeikumba Ghana. Huduma za afya katika taifa hilo la Afrika Magharibi inahusisha asilimia 38 ya wagonjwa wote, huku makundi ya wale walio katika mazingira hatarishi ni watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano.Shirka la Afya Duniani linasema mtoto anafariki kila dakika kutokana na malaria barani Afrika, ambako inakadiriwa vifo tisa kati ya kumi vya malaria vinatokea . Kuna matumaini kuwa chanjo mpya itawasaidia watoto wa Ghana na Afrika kupambana na malaria.
Dr. Nana Yaw Peprah mkuu wa program ya taifa ya kudhibiti malaria nchini Ghana ameiambia VOA kwamba chanjo ya Oxford imekuja kwa wakati muafaka.Karibu nusu ya idadi ya watu duniani iko katika hatari ya malaria. Mwaka 2020, inakadiriwa kuwa watu milioni 241 katika nchi 85 waliambukizwa malaria. Mwaka huo huo, WHO inasema ugonjwa huo ulisababisha vifo vya takriban watu 627,000.