Katika ziara yake ya siku tatu Voleker anatarajiwa kuwa na mikutano na watetezi wa haki za binadamu na mashirika ya jumuiya ya kiraia pamoja na rais Felix Tshisekedi na wajumbe wa serikali.
Volker alitembelea maeneo yaliyokumbwa na mashambulizi ya karibuni yakishutumiwa kutekelezwa na kundi la wanamgambo wa ADF linalojihusisha na Islamic state ambapo karibu raia 10 hadi 15 waliuwawa mwishoni mwa wiki katika wilaya ya Beni.
Kamishna huyo wa maswala ya haki za binadam wa Umoja wa Mataifa amesema “nimekutana na kundi la watu ambao wamekoseshwa makazi kutokana na ghasia mbaya, mauaji ya halaiki yalifanyika katika nyumba zao na wamekuwepo hapa kwa takriban miaka mitatu. Matarajio yao ni kurejea nyumbani.”