TEF imeahidi kuendelea kupinga vitendo vya uonevu vinavyofanywa dhidi ya vyombo vya habari, vikisema ni sehemu ya ukandamizaji wa uhuru wa habari na uvunjifu wa sheria, inayosimamia sekta ya habari nchini.
kwa mujibu wa vyanzo vya habari Tanzania, Mwenyekiti wa TEF, Theophil Makunga ametoa kauli hiyo Jumanne na kushauri uongozi wa gazeti hilo kwenda mahakamani kwa kuwa wanayo fursa ya kufanya hivyo.
Amesema uchambuzi uliofanywa na jukwaa hilo umebaini kuwa kifungu cha 59 cha Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016, kinatoa mamlaka kwa Waziri husika kuzuia maudhui katika habari na si kufunguia chombo cha habari.
Makunga amesema kwa kuzingatia uchambuzi waliofanya ni wazi kuwa mchakato ukiotumika kulifungia gazeti hilo umekiuka sheria.