Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 22:39

Mlipuko mkubwa waua 7, kujeruhi Mogadishu


Huu ni mlipuko wa mabomu ambao ulitokea hivi karibuni katika mgahawa huko Mogadishu.
Huu ni mlipuko wa mabomu ambao ulitokea hivi karibuni katika mgahawa huko Mogadishu.

Mlipuko mkubwa wa mabomu umeripotiwa Jumanne katika wilaya ya Wadajir, Mogadishu na kuua watu saba.

Mabomu hayo yaliripuka katika jengo la makao makuu ya Wadajir iliyoko upande wa kusini wa mji huo, katika majira ya saa 12:40 p.m baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo wameiambia VOA.

Basi dogo lililokuwa limesheheni mabomu liliripuka katika jumba la makao makuu ya Wadajir nakusababisha vifo na kujeruhi wengine, walioshuhudia tukio hilo wamesema.

Mwandishi wa VOA Mogadishu ambaye anaripoti kutoka kwenye eneo la mlipuko huo amesema aliona miili saba ya wale waliopoteza maisha.

Watu wengi wamefunikwa na kifusi na inatarajiwa kuwa idadi ya wahanga itaongezeka.

Mlipuko huu umetokea siku saba baada ya shambulizi la kinyama kutokea Kwenye Jumba la Mogadishu Pizza House ambalo liliuwa watu 29.

XS
SM
MD
LG