Wanajeshi wa Jeshi la Taifa ambao mashahidi wamesema wamepata nguvu hivi karibuni kutokana na kutumiya hivi karibuni ndege zisizo na rubani, droni, wamechukua udhibiti siku ya Jumanne wa makao makuu ya redio na televisheni mjini Omdurman, upandea wa pili wa mto Nile kutoka Khartoum na sehemu ya mji mkuu huo.
RSF, kundi kundi hasimu la kijeshi ambalo limekua linashinda katika mapigano hayo, limekua likilishikilia sehemu hiyo tangu siku za mwanzo za vita April mwaka jana.
Ingawa matangazo kutoka jengo la redio na televisheni yalisimamishwa, lakini kusonga mbele kwa jeshi katika mitaa ya kale ya kati ya Omdurman - ni mafanikio muhimu kimkakati kwa sababu inatumika kama makambi ya jeshi na kimekua kituo cha kupita vifaa vya kijeshi vya RSF.
Mashahidi wameliambia shirika la habari la Reuters kuwa wameona magari iliyoharibiwea ya RSF na miiili ya wapiganaji wake jirani na jengo a utangazaji siku ya Jumatano.
Jeshi litaendelea kupigana na RSF katika meneo mengine ya mji mkuu, na katika jimbo la Magharibi la Darfur jimbo la El Gezira kusini mwa Khartoum – maeneo ambayo RSF iliyateka kwa haraka mwaka jana “ mpaka ushindi kamili upatikane” Burhan alisema, kulingana na taarifa hiyo iliyotolewa Jumatano