Wakati ikiendelea na kampeni yake ya kuitokomeza Hamas katika Ukanda wa Gaza kwa mashambulizi ya anga na ardhini huko kaskazini, katikati na kusini mwa Gaza.
Taarifa ya Jeshi la ulinzi la Israel imesema limewakamata watu 21 na kuzuia mamilioni ya fedha za Israel katika operesheni huko Ukingo wa Magharibi.
Vikosi vya Israel pia vimefanya mashambulizi ya anga huko Jenin na wanajeshi wa ardhini walifyatua risasi kwa wapalestina wakijibu kile wanajeshi wanasema kuwa watu waliwafyatulia risasi wanaejshi wa Israel.
Shambulizi la ukingo wa magharibi lilikuwa la karibuni kufanyika kufuatia mfululizo wa operesheni ambazo zimefanywa na Israel, ikisema kuwa vikosi vyake vinafanya operesheni za kukabiliana na harakati za kigaidi.