Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 08:22

Benjamin Netanyahu ameapa kuongeza vita vya Israel dhidi ya Hamas


Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu

“Tunaongeza mapambano katika siku zijazo, na hivi vitakuwa  vita virefu na havijakaribia kumalizika”, alisema Netanyahu

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameapa kupanua vita vya nchi yake dhidi ya Hamas huko Gaza, wakati maafisa wa afya katika eneo hilo wakiripoti darzeni ya waathirika katika shambulizi la Israel kwenye kambi ya wakimbizi.

“Tunaongeza mapambano katika siku zijazo, na hivi vitakuwa vita vuirefu na havijakaribia kumalizika”, Netanyahu aliwaambia wanachama wa chama chake cha Likud siku ya Jumatatu. Mashambulizi ya Israel yalipiga kati-kati ya Gaza Jumapili jioni na Jumatatu.

Maafisa wa afya katika eneo linalodhibitiwa na Hamas wamesema watu wasiopungua 70 wameuawa katika shambulio la anga la Israel ambalo lilishambulia kambi ya wakimbizi ya Maghazi. Jeshi la Israel limesema linapitia upya mashambulizi yaliyoripotiwa huko Maghazi, huku likirudia ahadi yake ya kupunguza madhara kwa raia katika vita vyake ili kuliangamiza kundi la wanamgambo wa Hamas.

Ripoti za habari zinasema Misri inapendekeza mpango wa kumaliza mzozo wa sasa kwa kusitisha mapigano, kuachiliwa kwa mateka kwa awamu, na kuundwa kwa serikali ya Palestina ya wataalamu wa kusimamia Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi. Hakuna jibu rasmi kutoka kwa Israel au Hamas

kufuatia pendekezo hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG