Kishida alitoa hotuba yake wakati wa mkutano ambao Japan iliandaa pamoja na serikali ya Ukraine na kampuni za kibiashara mjini Tokyo. Zaidi ya makubaliano 50 ya ushirikiano yalitiwa saini na idara za serikali ya Japan na ukraine pamoja na makampuni. Waziri mkuu Denys Shynhal ameongoza ujumbe wa ukraine wa zaidi ya watu 100. Kishida amesisitiza umuhimu wa uwekezaji katika viwanda kwa ajili ya maendeleo ya baadae ya Ukarine. Japan inatarajia kujenga nguvu kusaidia ukraine wakati vita na Russia inaendelea.
Kishida pia ameahidi kurahisisha vibali vya kuingia Japan kwa watu wa Ukraine, wakati pia akitangaza kufunguliwa kwa ofisi ya Shirika la Biashara za Kigeni la Japan mjini Kyiv. Waziri mkuu wa Ukraine Denys Shmyhal amesema kuwa mataifa yote mawili yametia saini zaidi ya mikataba 50 ukiwemo ule wa kuzuia ulipaji ushuru mara mbili kati ya mataifa hayo, ambao ni muhimu kwa makampuni ya Japan yanayokusudia kuanza miradi ndani ya Ukraine.