Makubaliano yamepelekea baadhi ya misaada kibinadamu kuingia Gaza baada ya sehemu kubwa ya eneo la pwani lenye watu milioni 2.3 limekuwa kama nyika kutokana na wiki saba za mashambulizi ya Israel kulipiza kisasi shambulizi la mauaji la wanamgambo wa Hamas Octoba 7.
Wakati huo huo shambulizi la mauaji mjini Jerusalem lilikuwa ni ukumbusho muhimu kwa ghasia kusambaa.
Israel ambayo imedai Hamas iwaachilie walau mateka 10 kwa siku ili kuwezesha sitisho la mapigano kuendelea , imesema ilipokea orodha ya dakika za mwisho ya wale watakaoachiliwa leo na kuruhusu kusitishwa mpango huo wa kuanza tena mapigano alfajiri.
Hamas ambao iliwaachilia mateka 16 Jumatano wakati Israel imewaachilia wafungwa 30 wa paletsian pia imesema makubaliano yataendelea kwa siku ya saba.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken katika ziara yake ya tatu mashariki ya kati tangu vita ilipozuka alisema juhudi zilikuwa zinaendelea kwa ajili ya kuendeleza makubaliano.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.