Israel inasema haijaweka ukomo juu ya kiasi cha misaada ambayo itaruhusu kuingia Gaza, na inatuhumu mashirika ya misaada kwa kuchelewesha kufikisha misaada, lakini imekabiliwa na shinikizo kubwa hata kutoka kwa washirika wake wa karibu kufanya juhudi zaidi.
“Tunajaribu kuruhusu msaada kuingia kwa wingi, kuingiza msaada wa kibinadamu kwa wingi,” msemaji wa jeshi Amirali Daniel Hagari aliliambia kundi la waandishi wa habari wa kigeni.
Mapema Jumatano, jeshi lilitangaza kwamba lori sita za misaada zikiwa na chakula kutoka shirika la mpango wa chakula duniani ziliingia kwenye eneo la kaskazini la Ukanda wa Gaza, ambako janga la njaa limekithiri.
Kutakuwa na misafara zaidi kama hiyo kadhalika usambazaji wa misaada kutoka njia nyingine, na kufuatiwa na kudondosha misaada kutoka kwenye ndege na kupakua shehena za misaada baharini, Hagari alisema.