Iran imeripotiwa kulenga kuzalisha megawati 20,000 za nishati ya nyuklia kufikia 2041. Taifa hilo kwa sasa lina kiwanda kimoja cha nyuklia chenye uwezo wa kuzalisha megawati 1,000, na ambacho kilianza operesheni zake 2011 kupitia usaidizi wa Russia.
Iran pia inatengeneza kiwanda kingine chenye uwezo wa kuzaliza megawati 300 kwenye jimbo lenye utajiri mkubwa wa mafuta la Khuzenstan, karibu na mpaka wa magharibi na Iraq. Idara ya uangalizi ya Umoja wa Mataifa mwaka uliopita ilisema kwamba Iran imeongeza kasi yake katika kuzalisha uranium yenye uwezo wa kutengeneza silaha.
Mkuu wa idara hiyo ya IAEA, Rafael Grossi kupitia ripoti amesema kwamba Iran katika wiki za karibuni imeongeza uzalishaji wa uranium ya hali ya juu, ikiwa kinyume na hatua ya hapo awali ya kupunguza uzalishaji kuanzia katikati mwa mwaka jana.