Mwadiplomasia huyo wa Sweden aliitwa na msaidizi wa mkurugenzi wa wizara ya mambo ya nje anayehusika na Ulaya Magharibi, wizara hiyo iliandika kwenye mtandao wa X.
Ubalozi wa Iran mjini Stockholm ulikuwa tayari umekanusha tuhuma hizo siku ya Ijumaa kwamba Tehran ilikuwa inaajiri magenge ya wahalifu inayoyaunga mkono ili kutekeleza “vitendo vya uhalifu” dhidi ya maslahi ya Israel ndani ya Sweden.
Hilo limefanyika kama jibu kwa idara ya ujasusi ya Sweden iliyosema siku moja kabla kwamba Iran ilikuwa “inatumia mitandao ya uhalifu ndani ya Sweden kufanya vitendo vya uhalifu dhidi ya mataifa mengine, makundi au watu nchini Sweden inawaona kama tishio.”
Idara hiyo inayojulikana kama SAPO, ilisema vitendo hivyo vilikuwa vinalenga hasa “ maslahi ya Israel na ya Wayahudi nchini Sweden.”