Huawei yaendelea kukabiliwa na changamoto baada ya vikwazo vya Marekani

Simu ya Huawei smartphones

Mtaalam wa Uingereza, anayeunda vifaa maalum vinavyonasa mawasiliano, amesitisha uhusiano wake na kampuni ya mawasiliano ya Huawei, ili kuzingatia hatua ya Marekani kuifungia kampuni hiyo.

Hatua hii inaweza kumaliza uwezo wa kampuni ya Huawei kutengeneza vifaa maalum vya kunasa mawasiliano kwa simu zake za kisasa, itakazotengeneza baadaye.

Kampuni ya Huawei, sawa na Apple na watengenezaji wengine wa vifaa vya kunasa mawasiliano katika simu kama Qualcomm, zinatumia mfumo wa ARM kutengeneza vifaa vya usindikizaji ambavyo huwasha simu zake.

Kampuni ya Huawei imesema inathamini sana uhusiano wake wa karibu na washirika wake, lakini inatambua hali ngumu ambayo baadhi ya washirika wake wanapitia kutokana na maamuzi yanayochochewa kisiasa.

Marekani iliipiga marufuku kampuni ya Huawei, kununua bidhaa kutoka Marekani kuanzia wiki iliyopita, hatua iliyoathiri uhusiano wake na kampuni ya google inayotoa huduma ya uendeshaji wa mfumo wa simu zake kama gmail na ramani za google.

Marufuku hiyo pia inaathiri uhusiano wa Huawei na washirika wake wa vifaa vya kutengeneza simu.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.