Herzog akosoa madai ya kimbari dhidi ya Israel yaliyowasilishwa mahakama ya ICJ

Rais wa Israel Isaac Herzog

Rais wa Israel Isaac Herzog amesema leo kwamba hakuna jambo la kikatili na lisilo la kawaida kuliko kesi iliyowasilishwa katika mahakama ya kimataifa ya sheria ya ICJ ikishutumu Israel kwa mauaji ya kimbari dhidi ya wapalestina katika mashambulizi yake ya Gaza.

Kesi iliyowasilishwa na Afrika kusini inatarajiwa kuanza Alhamisi na kuzingatia zaidi vifo vya zaidi ya raia elfu 23 kulingana na maafisa wa afya wa Gaza vilivyotokea wakati wa vita vya zaidi ya miezi mitatu baina ya Israel na Hamas.

Akizungumza na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken , Herzog ameishutumu Afrika Kusini kwa unafiki kwa kuwasilisha kesi hiyo na kuishukuru Washington kwa uungwaji mkono wake kwa ajili ya Israel, ambayo inasema inafanya juhudi kuepusha majeruhi zaidi miongoni mwa raia wa Gaza.

“Kwa kweli maadui zetu, Hamas katika katiba yao wanatoa wito wa kuangamizwa kwa taifa letu la Israel, taifa pekee la wayahudi”, Herzog alisema”

“ tutakuwepo huko katika mahakama ya kimataifa ya sheria na tutawakilisha kesi yetu kwa kutumia misingi ya kujitetea wenyewe kutokana na haki zetu tulizozipata chini ya sheria ya kimataifa ya haki za binadamu,” aliongeza kusema.

Habari hii inatokana na shirika la habari la Reuters.