Hawaii: Kaunti ya Maui yatoa majina ya kwanza ya watu waliofariki katika ajali ya moto wa msituni

Kikosi cha utafutaji na uokoaji cha kitengo cha dharura cha serikali kuu FEMA kikiendelea na zoezi la kutafuta mabaki ya waathirika wa moto wa msituni Maui, Hawaii.

Kaunti ya Maui imetoa majina ya kwanza ya watu waliouwawa katika moto wa msituni ulioteketeza mji wa kihistoria wa Lahaina wiki moja iliyopita na kuongeza idadi ya waliofariki kufikia 106.

Ukubwa wa moto uliteketeza eneo la kilomita za mraba 13 za mji kwa saa kadhaa pamoja na changamoto za uokoaji zimeathiri wakaazi wengi wa Lahaina takriban 13,000 ambao pia wanakabiliwa na hasara ya kutopata dola za watalii zenye thamani .

Moto umeharibu karibu majengo 2,200 ambapo asilimia 86 ni makazi ya watu na kusababisha uharibifu wa dola bilioni 5.5 , maafisa wamesema.

Kwa mujibu wa white house takriban wafanyakazi 500 wa serikali kuu wamepelekwa MAUI. Ikulu inasema ni majibu ya haraka ya baada ya moto ambapo p[ia kikosi cha ulinzi wa pwani cha Marekani na jeshi la majini wanasaidia katika juhudi msako na uokoaji, wakati helikopta za jeshi la Marekani zinasaidia katika juhudi za kuzima moto huo katika jimbo hilo.