Hali tete baada ya jeshi la Sudan kuonya hatua ya wanamgambo kuanza kujikusanya

Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo.

Jeshi la Sudan limeonya kuwa kundi kubwa la wanamgambo linakusanya vikosi katika miji kote nchini.

Katika taarifa iliyotolewa mapema Alhamisi jeshi limekishutumu kikosi cha RSF kwa kuvunja sheria.

Hatua ya RSF kuvunja sheria, jeshi limesema katika maoni nadra kuhusu mzozo unaoendelea ambao umetatiza mpango wa mpito kuelekea demokrasia.

Kuna hofu kubwa ya kutokea mapambano kati ya pande hizo mbili.

Kiongozi wa RSF Mohamed Hamdan” Hemeti” Dagolo, alichukua jukumu muhimu wakati jeshi lilipochukua mamlaka nchini Sudan mwaka 2021.

Wiki hii viongozi walishindwa kufikia muda wa mwisho uliowekwa kuunda serikali ya kiraia.

Kuvunjika kwa mazungumzo hayo kumelaumiwa kutokana na tofauti kati ya makundi hasimu ya kijeshi.