Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:36
VOA Direct Packages

Raia wa Sudan waendelea kuitisha utawala wa kiraia miaka 4 baada ya kuondolewa kwa Bashir


Waandamanaji wa kuitisha demokrasia wakiwa kwenye mji mkuu wa Sudan, Khartoum, kwenye picha ya maktaba
Waandamanaji wa kuitisha demokrasia wakiwa kwenye mji mkuu wa Sudan, Khartoum, kwenye picha ya maktaba

Jumanne Aprili 11 ni miaka 4 tangu mapinduzi ya Sudan kufanyika, na kupelekea jeshi kumuondoa madarakani Rais Omar al Bashir.  

Kufikia sasa matumaini ya kujipatia utawala wa kiraia hayajatimia, huku. vuguvugu la kuitisha demokrasia nchini humo likiwa kwenye mvutano na jeshi kuhusu utawala. Kwa waandamanaji walioshiriki kwenye mapinduzi ya kumuondoa kiongozi huyo wa kijeshi wa miongo mitatu, Omar al Bashir, utawala wa kiraia kwao umebaki kuwa ndoto.

Oktoba 2021 baada ya miezi 18 ya utawala wa kiraia, kundi mpya la kijeshi lilifanya mapinduzi na linaendelea kutawala hadi sasa. Mohamed Ali ambaye ni mmoja wa viongozi wa maandamano ya karibu kila siku mjini Khartoum amesema kwamba jeshi linahitaji kuwa chini ya serikali iliyochaguliwa kidemokrasia.

Serikali ya kijeshi iliyopo Sudan kwa miezi mingi imesema kwamba itaweka mikakati ya kuunda serikali ya mpito kuelekea serikali ya kiraia. Rasimu ya makubaliano hayo ilikuwa itiwe saini Aprili 6, lakini hilo likaahirishwa dakika za mwisho. Wachambuzi wanasema kwamba viongozi wa kijeshi wanachelewesha mchakato huo ili waendelee kushikilia madaraka.

Cameron Hundson ambaye ni kutoka kituo cha masomo maalum anasema kwamba kadri jeshi linavyoendelea kuchelewesha mchakato huo ndivyo linavyoweka mikono yake kwenye mashirika ya kifedha ili kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia utakaokabiliana na shinikizo la ndani na nje ya nchi la kufanya mabadiliko.

Kamishna wa Umoja wa Mataifa kwenye masuala ya haki za binadamu Volker Turk ameelezea wasi wasi wake kutokana na hali ya taharuki ninayoendelea kutanda, wakati akiomba kubuniwa kwa mchakato mpya kuelekea kwenye utawala wa kiraia katika kutatua hali iliyopo.

XS
SM
MD
LG