Simulizi ya mwongozaji filamu wa Kiingereza Sam Mendes kuhusu Vita vya Dunia vya kwanza “1917” kutoka shirika la Universal Pictures ilishinda tuzo ya picha bora katika kundi la uigizaji na simulizi ya Quentin Tarantino ya Los Angeles "Once Upon a Time ... in Hollywood'' ilishinda tuzo ya filamu bora zaidi katika kundi la vichekesho au muziki.
Filamu zilizotarajiwa kushinda kama ya Martin Scorsese ya “The Irishman” kuhusu uhalifu na“Marriage Story,”ya Noah Baumbach ambazo zilitokea katika mtandao wa Netflix zilichukuwa tuzo moja kwa pamoja. Ilikuwa kwa msaada wa ushiriki wa Laura Dern kama wakili aliyeachika katika hadithi ya “Marriage Story,” ambaye alipita mvuto wa Jennifer Lopez kama mcheza densi machachari katika “Hustlers.”
“1917” ambayo itaanzwa kuonyeshwa kote nchini Marekani Ijumaa, pia ilishinda tuzo ya mkurugenzi bora zaidi kwa ajili Mendes. Filamu hiyo inawafuatilia wanajeshi wawili wa Uingereza kupitia mahandaki ya Vita Vya Dunia vya kwanza na imerikodiwa kuonyesha muendelezo wa masaa mawili.
“Natumai hii ina maana kuwa watu watajitokeza na kuiona filamu hii katika kumbi za sinema kama ilivyokusudiwa,” Mendes amesema
Filamu ya “Once Upon a Time…” ni hadithi iliyotokea katika wikiendi moja ya mwezi Februari mwaka 1969 iliyo kuwa inakusudia kuonyesha nguvu ya sekta ya filamu na maisha ndani ya Hollywood, ilichukuwa tuzo ya uandishi bora wa filamu kwaa Tarantino. Brad Pitt alishinda tuzo bora zaidi ya muigizaji msaidizi wa mchezaji filamu Leonardo DiCaprio's katika nafasi yake kama muigizaji wa matukio hatarishi katika filamu
Joaquin Phoenix, ambaye alicheza nafasi “Joker” katika filamu iliyo na jina hilo hilo, na Renee Zellweger, aliyecheza nafasi ya judy Garland katika filamu ya “Judy” ilichukuwa nafasi ya tuzo ya heshima ya ubora zaidi katika filamu ya vichekesho.
Taron Egerton (“Rocketman”) na Awkwafina (“The Farewell”) walikuwa washindi wacheza filamu wa mara ya kwanza katika eneo la vichekesho na muziki.