Gari la 'ajabu' la Apple laonekana Silicon Valley

Kampuni ya Apple

Wiki chache baada ya kupata kibali, gari la Apple linalojiendesha lenyewe limeonekana likizunguka katika mitaa ya Silicon Valley ambacho ni kituo kikuu cha utafiti wa technolojia Marekani.

Gari hilo aina ya Lexus lilowekewa aina mbalimbali za 'sensors’ la aina mpya limeingia katika soko la biashara lenye utashi wa magari ya aina hiyo ambayo hivi sasa yanawavutia sana wateja.

Apple, ambalo limekuja baadaye sokoni, linauwezekano wa kupata ushindani mkali, kwa kulikabili gari kama hilo aina jingine la Waymo la Kampuni ya Google, ambalo tayari limeshafanya majaribio kwa milioni ya maili barabarani, na kampuni ya Uber, ambayo imekuwa ikifanya majaribio ya magari yanayojiendesha yenyewe kwa miezi kadhaa sasa.

Juhudi za Apple, ambayo inajulikana rasmi kama mradi wa Titan, unaongozwa na mashine iliyotengenezwa na Velodyne Lidar, wakati Apple inatarajiwa kutengeneza mifumo ya kieletronikia.

Kwa mujibu wa nyaraka zilizopatikana kutoka kampuni ya Business Insider, Magari ya Apple yako kama magari mengine yanayojiendesha yenyewe.

Magari hayo “yanauwezo wa kupeleka amri za kieletroniki kwa ajili ya kutia kasi mwendo na kupunguza kasi na inaweza ikafanya sehemu ya majukumu ya kubadilisha kasi wakati iko katika mwendo,” kwa mujibu wa nyaraka hizo.

Kama ilivyo kwa magari mengine yasiyo na dereva, binadamu bado wanakuwepo na wanaweza kuingilia kati harakati za gari hilo wakati wowote.

Pamoja na kuwa linaonekana limechelewa kuingia sokoni, Apple inaweza kupata upenyo lakini kuna uwezekano wa kukabiliwa na mapambano marefu ya kisheria kati ya Waymo na Uber, na kuwa Waymo wanadai kuwa Uber iliwaibia siri zake za kibiashara.

Siku ya Alhamisi, Mkurugenzi wa Uber Anthony Levandowski alijitoa katika shughuli za utengenezaji wa magari yanayojiendesha yenyewe kufuatia kufunguliwa kwa mashtaka, yakidai kuwa alihusika na wizi wa haki miliki za kiufundi wakati alipokuwa ameajiriwa na Google.