Wanajeshi hao wamepelekwa kuulinda mji wa Washington katika hafla ya kuapishwa Biden wakati ukiwepo wasiwasi wa kuwepo shambulio la ndani lililohamasishwa na wafuasi wa Rais Donald Trump.
Waziri wa Ulinzi Ryan McCarthy aliwaambia shirika la habari la AP kuwa yeye na viongozi wengine hawajaona ushahidi wowote wa vitisho vyovyote.
Ameongeza kuwa hadi sasa uchunguzi wao haukuonyesha dalaili ya kuwepo matatizo yoyote kati ya wanajeshi hao.
“Tunaendelea kupitia mchakato huo, na kuchukua mtazamo wa pili, na wa tatu kwa kila mmoja aliopewa nafasi ya kushiriki katika operesheni hii," McCarthy alisema.
McCarthy alisema kuna ripoti za kiintelijensia zinazoonyesha kuwa kuna vikundi vya nje vinavyo andaa maandamano ya silaha kabla ya siku ya kuapishwa.