Familia zadai wanaoshikiliwa Korea Kaskazini wametelekezwa

Ji-Hyeon-A (Kulia), Mwanachi wa zamani wa Korea Kaskazini, akichangia katika kongamano linaloeleza uvunjifu wa haki za binadamu Korea Kaskazini

Familia za Wakorea Kaskazini wanaoshikiliwa wanajihisi kusahauliwa na Jumuiya za Kimataifa, licha ya kuongezeka taarifa ya kuenea kwa vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu nchini humo.

Hilo limeelezwa katika ripoti ya Umoja wa Mataifa ikisema kuwa uvunjifu wa haki za binadamu nchini Korea Kaskazini "uko katika kiwango hakijawahi kutokea katika ulimwengu huu wa kisasa."

Baba yake Hwang In-cheol's alikuwa kati ya abiria 47 na wafanyakazi wa ndege ya shirika la Korean – KAL – iliyokuwa imetekwa mwaka 1969 nchini Korea Kaskazini.

Lakini mateka hao 11 akiwemo baba yake Hwang, ambaye ni mwandishi wa habari na mkosoaji mkuu wa utawala wa Kim II, hawajaruhusiwa kurudi na hawana ruhsa ya kuwasiliana na familia yake.

"Mpaka hivi leo, miaka 48 imepita, baba yangu na watu wengine 11 ambao wanaendelea kushikiliwa kwa nguvu Korea Kaskazini na wamesahaulika," amesema Hwang, ambaye anaongoza kikundi cha utetezi cha wale wanaoshikiliwa kinachoitwa KAL Abductees' Repatriation Committee ambayo inajaribu kuleta muamko kwa vyombo vya habari kuhusu suala hili.

Baada ya vita vya Korea vya 1950-53, Korea Kaskazini iliwarejesha mateka wengi waliokamatwa wakati wa vita, lakini imeelezwa kuwa iliwalazimisha maelfu ya raia wa Korea Kusini kubakia nchini humo, kusaidia kujenga viwanda vya kitaifa, mashule vitu vingine vya msingi vinavyotumika vya taifa hilo. Baada ya miongo kadhaa kupita, maelfu ya watu zaidi waliripotiwa kukamatwa na Korea Kaskazini.

Wengi wao walikuwa wavuvi, waliochukuliwa kwa ajili ya kutoa habari za kijasusi au kutumika kwa ajili ya propaganda katika vita baridi inayoendelea katika Rasi ya Korea.