Hatua hiyo imekuja wakati serikali za Ulaya zikijaribu kukabiliana na tatizo la wakimbizi wanaondoka kwenye nchi zenye kivita barani Afrika na kutaka kuingia Ulaya kqwa kufanya safari hatari wakivuka bahari ya Mediterranean, ambapo mara nyingi zinaandaliwa na magenge ya uhalifu.
“Uamuzi huu unafuatia tathmini iliyofanywa na Tume, ambayo imehitimisha kuwa ushirikiano unaotolewa na Ethiopia katika kuwachukua tena raia wake ambao wanaishi kinyume cha sheria ndani ya Umoja wa Ulaya hautoshi” limesema baraza la EU.
Mapema mwezi huu, wabunge wa Ulaya waliidhinisha mfumo wa uhamiaji uliofanyiwa marekebisho.
Kituo cha kisiasa kinachoiunga mkono EU kimesema hii itapunguza idadi ya wahamiaji wanaowasili bila nyaraka rasmi, wakati ikitaka kuondoa mafanikio yaliyofanywa na kundi la mrengo wa kulia kabla ya uchaguzi wa wabunge mwezi Juni.