Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 03:33

Mflame Charles atoa idhini yake kuwa sheria mpango wa kuwapeleka waomba hifadhi Rwanda


FILE PHOTO: Mfalme Charles
FILE PHOTO: Mfalme Charles

Mfalme  Charles wa Uingereza ametoa idhini yake kuwa sheria mpango wa Waziri Mkuu Rishi Sunak kuwapeleka waomba hifadhi nchini  Rwanda.

Hili limetokea wakati jeshi la polisi nchini Uingereza likisema waliwakamata raia wa Sudan and Sudan Kusini ambao walikuwa wakiwasaidia uhamiaji haramu kuingia nchini humo.

Idhini ya Kifalme ni hatua ya mwisho katika mchakato wa sheria, na kwa ufanisi kupitisha uamuzi uliochukuliwa na bunge mapema wiki hii kuidhinisha mswaada baada ya malumbano ya muda mrefu kati ya serikali na wapinzani wa mpango huo.

Idhini ya Kifalme ilitangazwa na Bunge la Uingereza Alhamisi, ikimaanisha Mswaada wa Safety of Rwanda (Asylum and Immigration) hivi sasa utakuwa ni sheria.

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak

Bunge limeidhinisha sheria hiyo Jumanne asubuhi. Siku ya Jumatatu, Sunak alisema anatarajia ndege za kwanza kuelekea Rwanda zitaondoka katika muda wa wiki 10 hadi 12 baada ya sheria hiyo kupitishwa.

Wakati mamlaka za Uingereza zilisaini makubaliano hayo na Rwanda, polisi katika taifa hilo walitangaza kukamatwa kwa mtu mwingine, baada ya wahamiaji watano, akiwemo mtoto, kufariki wiki hii wakijaribu kuvuka kanali kutoka Ufaransa.

Idara ya Upelelezi ya Makosa ya Jinai ya Uingereza, NCA, ilisema imemkamata mtu mwenye umri wa miaka 18 kutoka Sudan Jumatano jioni kwa kushukiwa kusaidia uhamiaji haramu na kuingia nchini Uingereza kinyume cha sheria.

Baadhi ya taarifa katika repoti hii imetokana na mashirika ya habari ya Reuters na AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG