Orodha hiyo inajumuisha kundi la Tzav 9, ambalo EU imesema lilizuia malori kusambaza misaada ya chakula, maji na mafuta katika Ukanda wa Gaza.
Pia kwenye orodha hiyo, kuna Ben-Zion Gopstein, mwanzilishi na kiongozi wa kundi la Lehava, na Isachar Manne, ambao Umoja wa Ulaya umewaelezea kama waanzilishi wa makazi haramu katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu na Israel.
Wote wawili waliwekewa pia vikwazo na Marekani, kadhalika Tzav 9, ambalo Washington ilisema wiki iliyopita linapinga udugu wa Wayahudi na Wasio Wayahudi na kuwachukia Waarabu kwa sababu za kidini na usalama.
Waziri wa fedha wa Israel Bezalel Smotrich, mtetezi wa makazi ya walowezi, alivitaja vikwazo hivyo kuwa “hatua isiyofaa na isiyokubalika kati ya marafiki, na uingiliaji kati usio wa kidemokrasia katika demokrasia ya Israel ambayo inadhuru uhuru wa kujieleza na kuandamana miongoni mwa raia wa Israel.