Utaratibu huo mpya utairuhusu EU kuweka vikwazo kwa watu binafsi na taasisi zinazohusika na vitendo vinavyotishia amani , utulivu na usalama wa Niger, kudhoofisha utaratibu wa kikatiba au kujumuisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu au sheria za kimataifa za kibinadamu , baraza la EU limesema.
Kwa hili, EU inalenga kuangalia na kuimarisha hatua zozote zilizochukuliwa na taasisi wa kikanda ya Afrika Magharibi – ECOWAS.
“ Tangu mwanzo EU imelaani mapinduzi ya Niger kwa maneno makali,”mkuu wa sera za mambo ya nje wa EU Josep Borrell alisema.
“ Kwa uamuzi wa leo , EU inaimarisha uungwaji mkono wake kwa juhudi za ECOWAS , na kutuma ujumbe wa wazi kwamba mapinduzi ya kijeshi yana gharama.