Erdogan aonya kuwa ajenda ya Netanyahu inaweza kuleta 'maafa makubwa'

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan (kushoto) na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameonya kuwa ajenda ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu inaweza kusababisha "maafa makubwa" katika Mashariki ya Kati, na kuyataka mataifa ya Kiislamu kuchukua hatua.

Matamshi yake yalikuja huku wasiwasi ukiongezeka juu ya kuongezeka kwa vitisho na mapigano yanayoendelea kuvuka mpaka kati ya vikosi vya Israel na Hezbollah huko Lebanon vinavyoungwa mkono na Iran, na kuzua hofu kuwa huenda ikaingia katika vita kamili.

Shambulizi la Israeli katika shule huko katikaz kambi ya wakimbizi ya Al- Shati (beach), Gaza City.

Ghasia za mpaka wa Lebanon zilizuka baada ya wanamgambo wa Hamas kufanya shambulio ambalo halijawahi kushuhudiwa kusini mwa Israel, na kusababisha operesheni kubwa ya kulipiza kisasi ya Israel, inayoendelea.