ECOWAS huenda ikatuma majeshi Niger

Mkuu wa Majeshi wa Ghana, Makamu Admirali Seth Amoama akimkaribisha Mkuu wa Majeshi wa Ivory Coast Lassina Doumbia huko Accra Agosti 17 , 2023. Picha na GERARD NARTEY / AFP.

Wakuu wa kijeshi wa Afrika Magharibi wamekutana nchini Ghana siku ya Alhamisi ili kuratibu uwezekano wa uingiliaji kati kwa lengo la kubadili mapinduzi Niger.

Wakuu hao wana wasiwasi kwa msururu wa uvamizi wa kijeshi katika kanda hiyo, Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) wiki iliyopita iliamua kuanzisha upya

"kikosi cha dharura cha kurejesha utaratibu wa kikatiba" nchini Niger.

Jumuiya hiyo ya Afrika Magharibi iko tayari kuingilia kati kijeshi nchini Niger iwapo juhudi za kidiplomasia za kubadili mapinduzi hayo zitashindikana, afisa mwandamizi aliwaambia wakuu wa majeshi.

ECOWAS inawataka viongozi wa mapinduzi kumrejesha madarakani Rais Mohammed Bazoum, baada ya kuzuiliwa na walinzi wake Julai 26, ikionya kuwa inaweza kutuma wanajeshi kama suluhisho la mwisho.

Bendera za taifa za Niger na Mali zikiwa mezani wakati wa mkutano wa ECOWAS. Picha na GERARD NARTEY / AFP.

Maafisa wa jeshi wa Niger waliomuondoa madarakani Rais Mohamed Bazoum wamekaidi wito wa Umoja wa Mataifa, ECOWAS na mataifa ya Magharibi kumrejesha madarakani, jambo lililosababisha wakuu wa nchi za Afrika Magharibi kuamuru kuandaliwa kwa kikosi cha dharura.

"Demokrasia ndiyo tunayoiunga mkono na ndiyo tunayoihimiza," mkuu wa majeshi ya Nigeria, Jenerali Christopher Gwabin Musa, aliuambia mkutano wa umoja huo mjini Accra.

Wanajeshi wa ECOWAS wamekuwa wakiingilia kati migogoro mingine ya kikanda tangu mwaka 1990, ikiwa ni pamoja na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia na Sierra Leone.

Kuna maelezo machache yamejitokeza kuhusu uwezekano wa operesheni hiyo ya Niger, zaidi ya matarajio kwamba Ivory Coast, Benin na Nigeria kuchangia wanajeshi.

Nchi hizo – zote wanachama wa ECOWAS – tangu wakati huo wameshuhudia ukamataji madaraka wa kijeshi, kwa kiasi fulani kutokana msukumo unaochangiwa na hasira kwa serikali kushindwa kuzuia umwagikaji damu.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP na Reutres