Dunia Jumamosi inaadhimisha siku ya ujuzi wa Kazi kwa Vijana ambapo kauli mbiu ni kuwapa ustadi walimu, wakufunzi na vijana kwa mustakabali wa kuleta mabadiliko na kuangazia jukumu muhimu ambalo walimu, wakufunzi na waelimishaji wengine wanatimiza katika kutoa ujuzi kwa vijana kuingia katika soko la ajira na kushiriki kikamilifu katika jumuiya na jamii zao. Kutokana na hilo tunaungana na Gloria Anderson ambaye ni YALI Fellow na Mkurugenzi na mwanzilishi wa TEDI -Tanzania Enlightenment Development Innovations na anaeleza vijana wengi hawajapewa mazingira ya kupatiwa ujuzi ndio maana wanashindwa kupata ujuzi unaohitajika katika karne ya 21 katika bara la Afrika.
Dunia inaadhimisha siku ya ujuzi kwa vijana
Your browser doesn’t support HTML5
Dunia siku ya Jumamosi inaadhimisha siku ya ujuzi wa kazi kwa Vijana ambapo kauli mbiu ni kuwapa ustadi walimu, wakufunzi pamoja na vijana Kutokana na hilo tumezungumza na Gloria Anderson ambaye ni YALI Fellow na Mkurugenzi na mwanzilishi wa TEDI -Tanzania Enlightenment Development Innovations