Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Jumatano imetangaza kumalizika kwa mlipuko wa karibuni wa Ebola.
Mlipuko huo umedhibitiwa baada ya kuua takriban watu 55 katika muda wa miezi mitano iliyopita.
"Nimefuraha sana kutangaza kuwa mlipuko wa 11 wa virusi vya ebola katika jimbo Equater katika eneo kubwa la kaskazini magharibi mwa nchi umemalizika," Waziri wa Afya Eteni Longondo amewaambia wana habari.
Shirika la Afya Duniani limesema kuwa mlipuko wa karibuni uliuwa watu 55 miongoni mwa hao 119 walikuwa wamethibitishwa kuwa na maambukizi.
Imeongeza kuwa wengine 11 walikuwa wamefikiriwa kuwa na ugonjwa huo tangu mwezi June.