Maafisa wa polisi ni miongoni mwa kundi lililovamia jengo linalotumiwa na Ubalozi wa Ufaransa kwa lengo la “kumfukuza mwanadiplomasia wa Ufaransa”, wizara ya sheria ilisema katika taarifa.
Mwanadiplomasia anayehusika na ushirikiano wa kitamaduni kwenye Ubalozi alipigwa alipokuwa akishikiliwa kwa karibu saa tatu, huku wanadiplomasia wengine wawili wakisukumwa bila kupata majeraha”, chanzo cha kidiplomasia kiliongeza.
Wizara ya sheria ilisema “ Maafisa wa polisi na mfanyakazi wa ofisi ya mwendesha mashtaka ni miongoni mwa washambuliaji, na baadhi yao walikamatwa.”
Balozi wa Ufaransa Bruno Aubert alikutana na Rais Tshisekedi Jumatatu.
Waziri wa mambo ya nje wa DRC Therese Wagner Kayikwamba tayari alielezea masikitiko yake makubwa Jumamosi juu ya tukio hilo ambalo limekiuka mikataba ya kimataifa.