Watu wazima huko Equateur, Kivu Kusini na Sankuru, majimbo matatu yanayoathirika zaidi, ndio watapewa chanjo hiyo kwanza, kuanzia tarehe 2 Oktoba, Cris Kacita Osako, mratibu wa kamati ya Congo ya kukabiliana na Monkeypox, aliiambia AP.
Wiki iliyopita, shehena ya kwanza ya chanjo ya mpox iliwasili katika mji mkuu wa DRC, kitovu cha mlipuko huo.
Dozi 100,000 aina ya JYNNEOS zilizotengenezwa na kampuni ya Denmark, Bavarian Nordic, zilitolewa kama msaada na Umoja wa Ulaya kupitia idara yake ya majanga ya afya (HERA).
Dozi nyingine 100,000 zilitolewa mwishoni mwa Juma.
Dozi hizo 50,000 zilizotolewa na Marekani ni aina hiyo hiyo ya chanjo ya JYNNEOS.
Dozi hizo 250,000 ni kiwango kidogo sana kati ya dozi milioni 3 ambazo maafisa walisema zinahitajika ili kutokomeza mlipuko wa mpox nchini DRC. Nchi za Umoja wa Ulaya ziliahidi kutoa msaada wa zaidi ya dozi 500,000 nyingine, lakini ratiba ya usambazaji wa chanjo hizo bado haijawekwa wazi.