Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo jana Jumatano ilifanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya Kombe la Mataifa ya Afrika, baada ya kutoka sare ya 0-0 na Tanzania, matokeo ambayo yaliifanya timu Taifa Stars kuondolewa katika michuano hiyo.
Ilikuwa ni mara ya tatu ndani ya siku tatu kwa Wakongomani kutoka sare, na kuwafanya kumaliza katika nadfasi ya pili katika Kundi F, nyuma ya Morocco, ambao waliilaza Zambia 1-0.
DRC sasa itarejea katika mji wa pwani wa San-Pedro kwa mchuano wa hatua ya 16 bora dhidi ya Misri siku ya Jumapili.
Wakati huo huo, Tanzania inarejea nyumbani baada ya kupata pointi mbili pekee, na kumaliza ikiwa ya mwisho katika kundi hilo.
Timu hiyo haijawahi kushinda mechi yoyote ya kombe hilo la Mataifa ya Afrika, katika majaribio tisa, ambapo waliwahi kufika kwenye fainali mara tatu katika historia ya michuano ya AFCON.
Zambia pia wanfunga viragi baada ya kuonyeshwa kivumbi na Morocco.
Timu zote sasa zinachukua mapumziko ya siku mbili hadi Jumamosi.