DRC: Kampuni ya Microsoft yaanza kusaidia urasimishaji wa uchimbaji Cobalti

Wachimbaji madini wadogo wadogo DRC.

Kampuni kubwa ya programu za kompyuta duniani, Microsoft ilitembelea mgodi wa madini ya cobalti huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwezi Desemba.

Ziara hiyo ni kama sehemu ya hatua za awali za urasimishaji wa sekta hatari na yenye udhibiti mdogo ambayo wataalam wanasema ni muhimu kukidhi mahitaji ya malighafi kwa betri duniani.

Kongo inachangia robo tatu ya madini ya cobalti duniani. kiwango kikubwa cha madini yanayochimbwa Kongo ni Cobalt, lakini wachimbaji wadogo wadogo ambao huchimba kwa mikono, na mara nyingi kwenye machimbo, huchangia hadi asilimia 30 ya uzalishaji lakini kiwango hicho hubadilika kulingana na bei.

Ni ziara ya kwanza inayojulikana kufanywa na mtendaji mkuu wa Microsoft kwenye machimbo ya Cobalt nchini Kongo. Mkuu wa wafanyakazi wa technolojia na uwajibikaji wa kampuni Michele Burlington alikutana na wachimbaji huko Mutoshi, ambako kampuni ya Trafigura ilisaidia urasimishaji uliomalizika mwaka 2020.

Makampuni yanayotumia madini ya Cobalt kutengeneza bidhaa kuanzia magari ya umeme mpaka simu za kisasa yanapaswa kuboresha mazingira ya kazi katika machimbo ya wachimbaji wadogo badala ya ya kuwaondoa katika minyororo ya usambazaji, ripoti ya huru juu ya ziara hiyo ilidai Jumatano.

Cobalt

"Watengenezaji wa magari ya umeme na makampuni ya kielektroniki yanafanya kazi wakiwa jicho moja wazi na jingine limefungwa," alisema Dorothee Baumann Pauly, mkurugenzi wa Kituo cha Biashara na Haki za Kibinadamu cha Geneva, ambaye aliandika ripoti hiyo.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters