Shirika la habari la serikali ya China Xinhua, limeripoti kwamba rais Xi Jinping ameshuhudia hafla ya kusaini makubaliano ya kukarabati kilomita 1,860 katika ya China na Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia, TAZARA.
Marais wa Tanzania na Zambia pia walihudhuria utiaji saini huo. Viongozi hapo wako Beijing kuhudhuria mkutano wa China na viongozi wa nchi za Afrika.
Reli ya TAZARA ilijengwa kati ya m waka 1970 na 1975 kwa mkopo usiokuwa na riba uliotolewa na China.
Reli hiyo inatumika kusafirisha mizigo hasa madini ya almasi naCobalt kutoka Zambia na kupakiwa kwenye meli kwenye pwani ya Tanzania kuelekea masoko ya kimataifa.
Mnamo mwezi Februari, China alipendekeza kukarabati reli hiyo kwa gharama ya dola bilioni 1.
Darzeni ya viongozi kutoka nchi za Afrika wanakutana katika mji mkuu wa China, Beijing.
Mkutano huo unalenga kupata ufadhili kwa miradi mbali mbali ya ujenzi wa miundo msingi na mikataba ya biashara.