Chama tawala Zimbabwe chachuana na upinzani katika uchaguzi wenye utata

Kiongozi wa upinzani wa chama cha (CCC) Nelson Chamisa akipiga kura katika kituo cha kupigia kura kilichopo katika shule ya msingi ya Kuwadzana 2, Harare, Agosti 23, 2023. Picha na REUTERS/Philimon Bulawayo.

Matokeo ya awali ya kura za wabunge nchini Zimbabwe yanaonyesha kuwepo kwa mchuano mkali kati ya chama tawala na chama kikuu cha upinzani siku ya Ijumaa.

Katika uchaguzi huo ambao chama cha Rais Emmerson Mnangagwa cha ZANU-PF kilichokuwa madarakani kwa muda wa miaka 43, kinatarajiwa kwa kiasi kikubwa kuendelea kubaki madarakani.

Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe imesema bado inahakiki matokeo kutoka takriban vituo vya uchaguzi 12,500, na itaweza kuanza kutangaza matokeo siku ya Ijumaa. Matokeo ya kura za urais hayatarajiwi kutangazwa kwa siku kadhaa.

Zimbabwe ina historia ndefu ya uchaguzi wenye utata, kitu ambacho kinawafanya watu wengi kuwa na mashaka kuhusu matokeo rasmi ya uchaguzi huo.

Mnangagwa mwenye umri wa 80, anawania kuchaguliwa tena katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika ambayo inakabiliwa na mfumuko wa bei na ongezeko la ukosefu mkubwa wa ajira, huku Wazimbabwe wengi wakitegemea dola zinazotumwa na jamaa walioko nje ya nchi ili kujikimu.

Mpinzani wake mkuu ni wakili na mchungaji Nelson mwenye umri wa miaka 45 Chamisa.

Nafasi ya Zimbabwe ya kutatua mzozo wa madeni na kupata

mikopo kutoka Benki ya Dunia na Shirika la Kimataifa la Fedha iko hatarini, kwani wakopeshaji wa kigeni wamesema uchaguzi huru na wa haki ni masharti ya mwanzo katika mazungumzo yoyote yenye maana.

Serikali na tume ya uchaguzi zimeahidi kuwepo kwa uchaguzi usio na utata, lakini baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wamesema, kuna uwezekano mkubwa uchaguzi huo kuegemea upande wa Mnangagwa, ikizingatiwa historia ya chama chake kinachotumia taasisi za serikali kufanya udanganyifu wa matokeo.

Rais Emmerson Mnangagwa (kulia) wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi za chama cha ZANU-PF. Picha na Zinyange AUNTONY/AFP.

Polisi walifunga barabara karibu na kituo cha matokeo ya uchaguzi Ijumaa asubuhi, na wananchi walikuwa wakisimamishwa kuhojiwa, mwandishi wa shirika la habari la Reuters aliyekuwa mji mkuu wa Harare alisema.

Siku ya Ijumaa, waangalizi wa uchaguzi kutoka jumuiya ya kanda ya kusini mwa Afrika SADC walisema uchaguzi wa rais na wabunge nchini humo haujafikia viwango vya kidemokrasia.

Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SACD) ilitaja miongoni mwa baadhi ya masuala ambayo yameuharibu uchaguzi ni pamoja na kufutwa kwa mikutano ya vyama vya upinzani na madai ya manyanyaso kwa wapiga kura.

Hata hivyo, matokeo yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi hadi sasa yanaonyesha ZANU-PF ilishinda katika viti vya ubunge katika majimbo 38, na chama kikuu cha upinzani cha (CCC) kimeshinda viti 32, kati ya jumla majimbo 210 yenye mbunge mmoja kwa kila jimbo.

Matokeo ya awali yalionyesha ZANU-PF kinaendelea kushikilia katika ngome zake za maeneo ya vijijini, wakati CCC ilikamata kura za mijini, kama ilivyokuwa katika chaguzi zilizopita.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.