Salla, ambaye alichukua madaraka mwaka 2012 na hatawania muhula wa tatu madarakani, na hivyo kumtaja Ba kuwa mrithi wake, na uidhinishaji huo umethibitishwa na wajumbe wa chama cha Alliance for the Republic siku ya Alhamisi wakati wakimtaja mgombea wao kwa upigaji kura wa Februari.
“Kwa heshima kubwa nawaambia kwamba nimekubali kuwa mgombea wenu” Ba alisema katika hafla iliyofanyika katika hoteli moja mjini Dakar na kuhudhuriwa na wajumbe wa chama tawala na washirika wake.
Ba, mkaguzi wa zamani wa kodi, amehudumu katika wadhifa wa waziri mkuu tangu mwezi Septemba mwaka 2022. Kabla ya hapo alikuwa waziri wa mambo ya nje na waziri wa fedha.
Ba mwenye umri wa miaka 62, anaonekana na wachambuzi kuwa na uwezekano wa kushinda katika uchaguzi wa taifa hilo la Afrika Magharibi, lakini anakabiliana na wagombea wengine wengi.
ulinganan na taarifa za vyombo vya habari, kuna zaidi ya wagombea 200 ambao wanawania nafasi hiyo, akiwemo waziri mkuu wa zamani Mahammed Boun Abdallah Dionne na waziri wa mambo ya ndani wa zamani Aly Ngouille Ndiaye.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP