Hesabu ya mwisho ya kura ilionyesha chama cha Rais Cyril Ramaphosa kilipata wabunge 159 katika Bunge la taifa lenye viti 400, chini ya wabunge 230 na ulikuwa ushindi mdogo sana wa ANC katika uchaguzi mkuu.
Msemaji wa ANC Mahlengi Bhengu-Motsiri aliwambia waandishi wa habari kwamba chama chake kilifanya mazungumzo “ya kiuchunguzi” na vyama vingine kadhaa, huku kikijarabu kupata uungwaji mkono wa kutosha wa wabunge kuunda serikali na kumchagua rais.
.
Baraza la ANC la kufanya maamuzi linatarajiwa kukutana leo Alhamisi ili kuhakiki njia zote, ikiwemo kujaribu kuunda serikali ya wachache, alisema.
Lakini majadiliano yalijikita kwenye “serikali ya umoja wa kitaifa” kwa sababu hiki ndicho wananchi wa Afrika Kusini walichotuomba, aliongeza.