Matokeo yameonyesha Labour kitashinda viti 410 katika bunge lenye viti 650 na wingi wa viti 170, na hivyo kumaliza miaka 14 ya serikali inayoongozwa na chama cha Conservative.
Chama cha Sunak kinatarajiwa kupata viti 131 tu, chini ya viti 346 wakati bunge lilipovunjwa, ni matokeo mabaya ya uchaguzi kwa chama hicho katika historia yake.
Wapiga kura wamekiadhibu chama hicho kutokana na mzozo wa gharama ya maisha na miaka ya ukosefu wa uthabiti na malumbano ya ndani ya chama ambayo yamepelekea Uingereza kuwa na mawaziri wakuu wa tano tangu 2016.
“Mustakabali wa Uingereza ulikuwa kwenye kura katika uchaguzi huu. Na ikiwa tumefanya vizuri usiku huu, Labour kitaanza kufanya kazi mara moja kwa kuchukua hatua za kwanza kwa ajili ya mabadiliko,” Pat McFadden, mratibu wa kampeni ya chama cha Labour alisema katika taarifa.